Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano
Wakati mwingine wazee wa Israeli walipokwenda kumwuliza Ezekieli maswali, Mungu alisema na Ezekieli kuwa asipoteze muda kuwajibu (m.3, Bwana MUNGU asema hivi; Je! Mmekuja kuniuliza neno? Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sitaulizwa neno na ninyi). Ila tu awasaidie kuondoa dhana mbaya waliyokuwa nayo juu ya Mungu. Kila wakati unapoulizwa swali juu ya imani yako, mwulize Mungu kama ni sawa kumjibu kila mtu swali analouliza. Maana Mungu aweza kukutaka kuwafanyia uinjilisti kwanza ili wamjue Mungu wetu. Wapo watu wanaotetea uovu na dhambi, wasikupotezee muda, waombee Mungu aseme nao.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz