Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

SIKU 16 YA 30

Kwa kutafakari m.8-12 tunajuzwa mwelekeo wa Elihu. Anaona Ayubu hana haki akisema Mungu humhesabu kuwa ni adui yake (m.10, Hunihesabu kuwa ni adui yake). Ila Elihu hamhukumu Ayubu wala kumwagiza atubu, bali anatafuta kumhakikishia kwamba Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu (m.12)! Tujifunze hapo. Mara nyingi sisi ni kama viziwi Mungu akiongea nasi. Hatujali akisema kwa namna iliyo tofauti na tunavyofikiri (ling. m.14 ilipoandikwa, Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali). Katika Biblia njia ya Mungu hujulikana kwa wamwaminio. Hapo tunajifunza kuwa majaribu hayaui ila huimarisha.

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz