Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021Mfano
Kwa nini Elihu anathubutu kunena wakati wazee wale watatu wameishiwa neno kwa Ayubu? Kwa nini anajiona kuwa na jawabu la yanayomkabili ateswaye? 1) Anahimizwa na Roho wa Mungu. Katika m.18 anasema, Nimejaa maneno; Roho iliyo ndani yangu hunihimiza. Na katika m.4 anaendelea kumsifu Roho wa Mungu kama huyu anayemwezesha, Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai. 2) Ni msema kweli bila kuficha (m.3, Hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu). 3) Anajiweka katika kiwango alicho nacho Ayubu mbele ya Mungu (m.6, Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe; Mimi nami nilifinyangwa katika udongo). 4) Hana kusudi baya. Sitakulemea kwa uzito, anamwambia Ayubu katika m.7. Basi, Ayubu asiogope. Wakati hao wazee walihukumu tu, maoni ya Elihu juu ya hali ya Ayubu ni mapana zaidi. Hivyo Elihu ni chombo kinachofungulia kwa Mungu kujifunua.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz