Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

SIKU 5 YA 30

Siku hii ya pili ya sikukuu ya Pasaka ni siku ya kutembea na Yesu aliyefufuka. Sikukuu hii huambatana na utume wa Kristo Yesu anayewatuma na kuwapa mamlaka wanafunzi kwenda kuipeleka Injili: Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi (m.21). Kama alivyotangaza amani kwa waliokuwa na hofu baada ya kifo chake, hata leo Yesu bado anatangaza amani kwa watu wote, hata wale wanaolemewa na mizigo ya dhambi. Leo Yesu anajifunua kwako kwa kupitia Neno lake. Fungua moyo wako ili aingie na kufanya matengenezo moyoni mwako. Mwaliko wake ni wazi: Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha (Mt 11:28).

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz