Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano
"Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie" (m.30). Maana yake ni kwamba ishara zote zilizosemwa na Yesu na manabii zilianza kutukia tangu kipindi kile na bado zinaendelea. Inayobaki ni kurudi kwa Yesu. Kwa hiyo tukeshe na kuomba ili tuwe tayari wakati wote, kama Yesu anavyosema katika m.33, Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo. Kwa njia hii Yesu anatufundisha kujiandaa sasa. Lakini wakati wa ujio wake hakuna ajuaye. Basi, wakati tunaendelea kumsubiri Yesu, tuendelee na utume aliotuagiza wa kutangaza Injili kwa watu wote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz