Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano
Tulijifunza katika somo la jana kwamba Daudi alitambua kuwa kimbilio liko kwa Bwana Mungu tu. Baada ya kutambua haya Daudi aliendelea kumsifu Mungu kwa utukufu wa kazi yake kwa wanadamu. Kwa ujumla Zaburi ya 40 ni zaburi ya sifa na utukufu kwa Bwana kwa yale aliyotutendea. Ieleweke kwamba, anayemsifu Mungu si lazima aelezee raha anayoipata tu. Bali katika sifa zake anayo hata nafasi ya kumwambia Mungu yale yanayomkosesha amani: Mabaya yasiyohesabika yamenizunguka mimi. Maovu yangu yamenipata, wala siwezi kuona. Yamezidi kuliko nywele za kichwa changu, na moyo wangu umeniacha (m.12). Kwa hiyo anaomba: Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa, Ee Bwana, unisaidie hima (m.13). Tuendelee kumsifu Mungu kwa kazi yake kwetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz