Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano
Madhumuni ya Mungu kutenda hayo yote yaliyotabiriwa katika Eze 38-39 ni ili watu wote wajue Mungu ni mtakatifu. Ndiye BWANA anayestahili kuaminiwa na wote. Pia tujue kuwa uovu utaangamizwa kabisa. Wakati Israeli mpya litakapojengwa na Mungu, atamwangamiza Gogu moja kwa moja. Hivyo uovu wote utakuwa umepata mshahara wake, na watu wa Mungu watasahau aibu yao na uasi walionitenda, anaahidi Mungu (m.26 BHN). Tangu siku hiyo na baadaye (m.22) itakuwa hivyo milele. Rudia m.28-29 ukitafakari ujumbe wake: Watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wao, kwa kuwa naliwahamisha, waende utumwani kati ya mataifa, na mimi nikawakusanya, na kuwaingiza katika nchi yao wenyewe; wala sitawaacha tena huko kamwe, hata mmojawapo; wala sitawaficha uso wangu tena; kwa maana nimemwaga roho yangu juu ya nyumba ya Israeli, asema Bwana MUNGU.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz