Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano
Njoni, enyi wana, mnisikilize, nami nitawafundisha kumcha Bwana (m.11). Sasa Daudi anasema na waumini kama wanafunzi wake. Anasisitiza umuhimu wa kutenda mema na kuachana na mabaya. Mtu wa Mungu awe mtu wa kutafuta amani, ukaifuatie (m.14). Hili ni jibu kwa swali katika m.12: Ni nani mtu yule apendezwaye na uzima, apendaye siku nyingi apate kuona mema? Yesu anasema: Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu (Mt 5:9). Fundisho lingine ni kwamba ukiwa umevunika moyo, Bwana yu karibu nawe (m.18)! Fundisho muhimu pia ni hili: Mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini Bwana humponya nayo yote (m.19; ukipenda soma pia Rum 8:35-39). Hakika Bwana yu mwaminifu kwetu!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz