Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano
Wayahudi walimpokea Yesu kwa shangwe kuu alipoingia Yerusalemu. Walitegemea atakuwa mfalme atakayewaokoa katika mateso, na hasa jambo lile la kutawaliwa na Warumi. Kupanda punda kulimaanisha Yesu ni Mfalme wa Amani, na pia kunadokeza utimilifu wa unabii wa Zak 9:9 unaosema, Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda. Maana ya neno “Hosana” ni "Bwana utuokoe". Walikuwa tayari kumpokea Yesu kwa kutandika nguo zao na matawi ili apite. Kwa sasa anataka aingie ndani ya moyo wako kama Mfalme wa Amani. Je, upo tayari kufungua moyo wako ili Yesu aingie?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz