Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano
Wayahudi walizifafanua amri kumi za Mungu zikawa zaidi ya mia sita. Swali lao kwa Yesu ni: Kati ya amri hizi ipi ni kubwa? Amri zina sehemu kuu mbili. 1. Amri za kwanza (amri 1-3 au 4; inategemea jinsi sisi wa siku hizi tunavyohesabu) zahusu uhusiano kati ya mwanadamu na Mungu. 2. Amri za mwisho (amri 4 au 5-10) zahusu mahusiano ya mwanadamu na jirani yake. Na jambo kuu pande zote mbili ni upendo. Upendo ni alama ya Mkristo. Wewe je, maishani mwako unasimamia sheria fulani ndogondogo kuliko jambo hili kuu? Kuna hatari ya kuishi hivyo! Zingatia maneno ya Yesu katika Mt 23:23-24, Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz