Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

SIKU 7 YA 31

Viongozi walikuwa na mavazi ya kipekee ili wapate heshima na salamu maalumu. Katika masinagogi walikaa viti vya mbele ili waonekane na watu. Ni hatari tukipenda kusifiwa na watu wakati kwa Mungu hatuna sifa. Binadamu kwa ujanja hujipendekeza, lakini Mungu anajua mioyo yetu. Kwa mfano yule mjane, hakuthaminiwa na watu, ila kwa Yesu ni wa thamani. Sadaka yake haimaanishi tutoe kidogo, bali kwanza tujitoe mioyo yetu kikamilifu kwa Mungu. Ndipo tutoe sadaka kwa kadiri tunavyojaliwa na Mungu.

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz