Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano
Mwaka 168 KK mfalme wa Kiyunani aliwashinda Wayahudi akajenga madhabahu ya kipagani hekaluni huko Yerusalemu. Hiyo yawezekana ni utimilifu wa Dan 9:25-27 inayosema, Ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu. Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa. Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu. Lakini Marko akiongeza ”asomaye na afahamu” (m.14) kwa habari ya chukizo la uharibifu, inawezekana anafikiria ile hali ya watu kuacha kumtegemea Mungu na kuwatumainia wanadamu na mali. Lakini licha ya kuwepo kipindi kigumu cha watu wa Mungu, Yesu atakuja mara ya pili kuhukumu watu. Na wateule watakutanika mbinguni. Je, wewe umejiandaa?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz