Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano
Bado viongozi wanafikiri elimu yao inawawezesha kutega mitego ya kumnasa Yesu ili ashtakiwe. Wayahudi walipaswa kulipa kodi kwa Kaisari. Na hata sisi tusikwepe kodi. Swali la Masadukayo linahusiana na utamaduni wao wa kurithi mke wa ndugu aliyekufa bila kuacha mtoto. Wanasema: Kama wamerithiana ndugu saba, je, mke huyo baada ya ufufuo atakuwa wa nani kati ya wale saba? Yesu anawaambia kuwa tatizo lao ni kutokumfahamu Mungu na Neno lake. Maana hakuna kuoa wala kuolewa baada ya ufufuo wa wafu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz