Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

SIKU 3 YA 31

Viongozi wa dini ya Kiyahudi walipomwuliza Yesu maswali, mara nyingi aliwajibu kwa maswali. Tendo la Yesu kusafisha hekalu liliwaudhi sana. Dai lao kubwa ni kwamba mamlaka aliyo nayo amepewa na nani? Tatizo lao ni kujiona ni wenye haki wakati maisha yao yanapingana na ukweli wa Neno la Mungu. Swali la Yesu kwao lina mamlaka ya kimungu, hivyo linawahukumu. Badala ya kutubu wanakwepa ukweli na kutumia uongo. Hili ni tatizo kubwa kwa watu wengi. Je, wewe unafanyaje Neno la Yesu linapokuchoma?

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz