Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano
Mikononi mwako naiweka roho yangu (m.5a). Jambo hili ni kilele cha mambo aliyoyafanya Mwimba Zaburi kwa Bwana wakati wa mateso. Yaliyotangulia ni kumkimbilia na kumwomba Bwana (m.1, Nimekukimbilia Wewe, Bwana; na m.2, Unitegee sikio lako, uniokoe hima. Uwe kwangu mwamba wa nguvu, nyumba yenye maboma ya kuniokoa). Na Bwana ana fadhili nyingi. Aliona mateso yake akamkomboa ili Mwimba Zaburi afurahie fadhili za Bwana, kuzidi kumtumainia na kuchukia uovu. Je, wewe unafanya kama Mtunga Zaburi? Ili kukombolewa na kushindi uovu, njia yetu ni kumkimbilia, kumwomba na kumkabidhi Bwana roho zetu. Tafakari tena m.1: Nimekukimbilia Wewe, Bwana, nisiaibike milele. Kwa haki yako uniponye!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz