Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021

SIKU 10 YA 30

Daudi anamtolea Bwana sifa nane (jabali, ngome, mwokozi, mwamba, ngao, pembe ya wokovu, manara, makimbilio; m.2-3). Huonyesha jinsi alivyompenda na kumtegemea Bwana katika maisha yake: Katika shida yangu nalimwita Bwana ... naye akaisikia sauti yangu hekaluni mwake (m.7), maana Mungu ndiye aliye hai (22:47)! Tufuate mfano wa Daudi. Tuombe katika jina la Yesu, nasi tutajifunza ndiye Mungu aliye hai! Vita yetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho (Efe 6:12). Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani (1 Petro 5:6-9).

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/