Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021Mfano
Daudi anafurahia ushindi ambao Mungu alimpa juu ya adui zake. Ndivyo Mungu alivyokuwa amemwahidi, kama ilivyoandikwa katika 7:9-11, Nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina kuu, kama jina la wakuu walioko duniani. ... nami nitakustarehesha mbele ya adui zako wote. Katika hili Daudi pia ni mfano wa Kristo. Kwanza yametimizwa kwa njia ya Injili kuhubiriwa duniani pote. Hivyo watu wa mataifa yote wametubu na kumkiri Kristo. Katika m.44-45 Daudi anamwambia Bwana, Umenihifadhi niwe kichwa cha mataifa ... Wageni watanijia wakinyenyekea; kwa kusikia tu habari zangu, mara watanitii. Ndivyo ilivyotokea kwa Yesu alipowatuma wanafunzi wake, akisema, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi. Pili yatatimizwa wakati Kristo atakapokuja mara ya pili kuuhukumu ulimwengu. Katika m.39-40 Daudi anamwambia Bwana, Wameanguka chini ya miguu yangu. ... Umenitiishia chini yangu walioniondokea. Ndivyo itakavyotokea kwa Yesu, kama ilivyoandikwa katika 1 Kor 15:24-28, Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo. Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/