Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021Mfano
Tauni (m.15) ni ugonjwa unaoambukizwa na viroboto vya panya. Daudi alipokutana na yule malaika wa Bwana na kumwona kwa macho ndipo akatambua zaidi ubaya wa kosa lake. Tazama, ni mimi niliyekosa, ni mimi niliyepotoka (m.17; katika 1 Nya 21:16-18 maneno ya Daudi yamenukuliwa kwa urefu zaidi, Je! Si mimi niliyeamuru watu wahesabiwe? Naam, mimi ndimi niliyekosa, na kufanya yaliyo maovu sana; lakini kondoo hawa, wamefanya nini? Mkono wako, nakusihi, Ee Bwana, Mungu wangu, na uwe juu yangu, na juu ya nyumba ya babangu; wala si juu ya watu wako, hata wao wapigwe). Tunapokutana na utukufu na usafi wa Bwana katika maisha yetu tunaona kwa wazi zaidi dhambi zetu na kupotoka kwetu. Ndipo hofu ya Bwana inakuja juu yetu. Kwetu sisi msaada ni madhabahu ya Golgotha, yaani, kifo cha Yesu kwa ajili yetu. Kuhusu Daudi imeandikwa katika m.25 kwamba akamjengea Bwana madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Basi Bwana aliiridhia nchi, na tauni ikazuiliwa katika Israeli. Kuhusu Yesu imeandikwa katika 1 Yoh 1:5-9 kwamba tukienenda nuruni, kama [Mungu] alivyo katika nuru, ... dau yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/