Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021Mfano
![Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F28523%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Bwana akafanya wokovu mkuu siku ile (m.10, 12). Ni wazi kwamba Daudi alipokuwa mfalme, Bwana ndiye aliyepewa sifa zote jeshi lilipokuwa limeshinda juu ya adui zao! Lakini pia ni wazi kwamba katika kuwapa ushindi, Bwana alitumia watu hodari na mashujaa. Ni habari za watu hawa tunapata leo. Jumla yao hapa ni watu 37 (m.39). Kwa kawaida waliitwa tu wale thelathini (m.13, 24). Katika m.18, 19a na 22 pameandikwa “watatu”. Badilisha na neno thelathini; hiyo ni tafsiri nzuri zaidi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F28523%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/