Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021

SIKU 8 YA 30

Kwa tendo gani nifanye upatanisho, mpate kuubariki urithi wa Bwana? (m.3). Jibu linapatikana katika m.2. Sauli alikuwa amevunja kiapo cha Yoshua kwa kuwaua Wagibeoni. Yoshua akafanya amani pamoja nao, na kufanya agano nao, ili kwamba waachwe hai; na wakuu wa mkutano wakawaapia (Yos 9:15). Hivyo Wagibeoni walishindwa kuwatakia baraka Waisraeli. Uovu ulihitaji kupatanishwa ili kuondoa njaa ya nchi. Kwa kufuata sheria ya Musa katika Hes 35:31-33, wanaume saba wa ukoo wa Sauli waliuawa (msipokee fidia kwa ajili ya uhai wa mwuaji, ambaye amekuwa na hatia ya mauti; Lakini lazima atauawa). Kwetu sisi Yesu ni Mpatanishi kwa kifo chake msalabani. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote (1 Yoh 2:1-2)! Hivyo sheria hii ya Musa imefutwa, na tufuate mafundisho ya Yesu kuhusu kutolipiza kisasi na kuwapenda adui zetu kama yalivyoandikwa katika Mt 5:38-48! 

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/