Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Farao aliona mapigo ya Mungu akakaidi. Wanadamu walio na chapa ya mnyama hufanana naye. Mateso yao hutokana na hasira ya Mungu, lakini hawatubu wala kumpa utukufu. Wanadamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu (m.9), bali wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao (m.11). Hudanganyika wanapochochewa na zile roho za mashetani zinazojiingiza kupingana na Mwenyezi (m.14, Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakunayanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi). Kinyume chao ni waumini. Wamevikwa vazi la haki kama alama ya kuwa wamepatanishwa na Mungu. Lililobaki kwao ni kufanya wanavyoonywa na Yesu, Bwana wao: Wakeshe na kutunza haki waliyopewa na Mungu kwa neema yake (m.15).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/