Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021

SIKU 1 YA 31

Wakati baragumu (8:7nk) zilileta mapigo juu ya theluthi tu, hukumu ya Bwana itakuwa imekamilika baada ya vitasa kumiminika, nayo ni ya haki (taz mist.5, 6 na 7 inayokaza kuwa watakaohukumiwa wamestahili, na Mungu yu mwenye haki ambaye hukumu zake ni za kweli na za haki). Maana daima Mungu hutanguliza neema yake iokoayo kwa wanadamu. Paulo anaeleza zaidi akisema, Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema (Tit 2:11-14). Kwa hiyo tunaposoma leo habari ya mapigo kabla hayajatokea, ni mwaliko na njia ya Mungu ili wanadamu waghairi na kuacha maovu yao. Ni nafasi ya mimi na wewe kumgeukia Mungu hata pasipo kungoja mapigo. Mwamini Yesu sasa; anaweza kusamehe na kuponya.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana