Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Mali, fahari na mamlaka za kidunia zaweza kuteketea ghafla katika majanga ya asili au vita, lakini katika somo hili sababu ni hukumu ya Mungu. Itaziondoa anasa hizo katika saa moja tu! Angalia huzuni ya wote walioishi katika mfumo wa maisha wa kibabeli na kujitenga na Mungu. Wanaomboleza vile vitu tu walivyokuwa navyo binafsi; hawafikirii hasara yao ya kweli, yaani kupoteza nafsi (Mk 8:36), wala hawatubu. Hivyo huthibitisha hukumu ya Mungu kwamba ni ya haki. Sisi je, tunatiwa huzuni gani tukisoma habari hizo?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/