Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Ile Haleluya (19:1) inaendelea. Sasa ni zamu ya yule adui mmoja ambaye habari ya hukumu yake haijasimuliwa bado, yaani shetani. Je, miaka 1000 ni mfano wa kipindi cha Injili kuhubiriwa? (Wanaosema ‘ndiyo’ huonesha Ufu 20:7-10 ikilingana na 16:14-16 na 19:19-21.) Au ni kipindi cha utawala wa miaka 1000 wa Kristo pamoja na waliouawa kwa sababu hawakupokea chapa ya mnyama, ambayo itafuata mpinga Kristo kuhukumiwa? Wakristo waona tofauti. Lakini angalia kuwa somo lote ni mpango wa Mungu unaotimia. Huo hauna wasiwasi!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/