Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Hekaluni, Patakatifu pa patakatifu palikuwa pa mraba ili kulingana na jambo halisi la mbinguni. Ni kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema (Ebr 8:5). Yerusalemu mpya ulio wa mraba ndio jambo hilo! Ukubwa wake hulingana na idadi ya watu wa Mungu (Ufu 7:4; Yohana aliandika ”stadia 12,000” badala ya ”maili 1,500”, na 12 x 12,000 ni 144,000). Yaani, somo la leo ni maono juu ya makazi yenye ukamilifu ya watu wa Mungu waliokamilika, sawasawa na ahadi ya Yesu kwamba, Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; ... maana naenda kuwaandalia mahali (Yn 14:2). Jitahidi uingie mji huu, maana ni uzuri ulioje kuingia ndani!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/