Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Duniani tumezoea kujijengea mahekalu na makanisa. Pia jambo la nishati ya kutupatia mwanga na joto hutushughulisha sana. Katika mji wa Yerusalemu wa mbinguni, hamna jengo la kuabudia wala jua. Mahitaji yote yamesawazishwa na uwepo wa Mungu. Atosha kama hekalu na nuru. Hofu ya giza imekoma. Ipo tu nuru ya Mungu inayowaangazia mataifa hata waweze kumheshimu na kumtukuza mchana na usiku. Mwisho kuna onyo kwamba, ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo (m.27). Zingatia na kufuata onyo hilo, ili usije ukakosa kuingia mji huu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/