Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021

SIKU 22 YA 31

Mara ya pili Bwana Yesu anakaza: “Naja upesi.” Kuja kwake kuna tokeo kwa wote: Kwao wayashikao maneno yake, wakizifua nguo zao katika damu yake, Yesu atawapa ujira wa neema, maana atawapa uzima wa milele nao ni bure (m.17, Yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure). Lakini kila mtu apendaye uongo na kuufanya, ujira wake utakuwa adhabu ya milele pamoja na shetani (Ufu 21:8, Waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti). Ila upo bado mwaliko wa kifalme: “Njoo!” Waumini wote (= Bibi-arusi) watumie muda mfupi wa neema uliobaki kutangaza mwaliko huo ili mwenye kiu asikose uzima.

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana