Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Mfiadini ni mtu anayekubali kutetea Ukristo kwa kufa kwa ajili ya imani yake. Katika Biblia kuna watu wengi waliokubali kufa hivyo; miongoni mwao Stephano huhesabiwa kuwa wa kwanza. Kumbuka, Bwana Yesu alikufa kwa ajili ya kuwaokoa wanadamu mikononi mwa shetani. Je, tunajifunza nini? Yohana anatukumbusha, uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima (Ufunuo 2:10b). Sisi leo pia tuwe tayari kuutetea Ukristo. Kila mmoja wetu na awe tayari kuvumilia magumu yote kwa sababu ya imani. Kama upo tayari kuteswa kwa ajili ya Kristo, Mungu akubariki kwa utayari wako.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/