Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021

SIKU 30 YA 31

Zaburi hii inamsifia mtu ambaye si wa kawaida. Wakati unaposoma zaburi hii jiulize maswali kadhaa: Ni nani ambaye ni mzuri sana kuliko mwanadamu, ambaye neema imemiminwa midomoni mwake? Ni nani ambaye ameipenda haki na kuichukia dhuluma, ambaye Mungu amempaka mafuta, mafuta ya furaha kuliko wenzake? Ukiichunguza zaburi hii kiroho, utagundua kuwa picha hii inamhusu Yesu na Kanisa lake. Yesu Kristo ndiye mtu pekee aliyeishi duniani akiwa katika hali zote za kibinadamu, lakini hakutenda dhambi.

siku 29siku 31

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/