Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Mungu aliufanya ulimwengu kwa njia ya Mwana wake, Yesu, na kumweka kuwa mrithi wa yote. Mungu yuleyule aliyezungumza zamani kwa kutumia manabii na kwa njia nyingi, mwisho ameamua kuzungumza nasi kwa njia ya Mwana huyo. Yesu akisema, ni Mungu anayesema. Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu kwa jinsi ya kimwili (Kol 2:9). Pia huyu Mwana alikuwa Kuhani wetu, akatufanyia utakaso wa dhambi zetu kabla ya kurudi kwa Baba. Ndiyo maana Yesu alisema, Aliyeniona mimi amemwona Baba (Yn 14:9). Unatakiwa Krismasi njema.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/