Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Mbinguni, uzima ni tele. Huchotwa kama maji toka mtoni. Kuupata hakuna foleni. Magonjwa hayapo, maana uzima ni wa milele, na uponyaji humea kama mti uzaao matunda kila wakati. Ni uzima na afya tele! Hofu na giza havipo Mbinguni. Maana hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote (Yn 1:18), lakini sasa ahadi ya kumwona imetimia maana tutafanana naye; ... na tutamwona kama alivyo (1 Yoh 3:2). Halafu nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao (Ufu 22:4)! Ndiyo uzuri na ukamilifu wa jinsi hii ambao Mungu amewakusudia wote awapendao. Na bado nafasi ingalipo kwa kila atakaye kumwamini Yesu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/