Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Yohana akionyeshwa yule Bibi-arusi ambaye ni mfano wa wote wampendao Yesu, anauona Yerusalemu mpya (ling. m.9 na 10 ilipoandikwa kwamba yule malaika anataka kumsaidia Yohana kumwona yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo, na Yohana anapoangalia anaona ule mji mtakatifu, Yerusalemu). Ni wenye utukufu, uzuri na ukamilifu wote. Hamna msongamano na machafuko kama katika Babeli ya watu waovu na wakatili iliyokwisha kuhukumiwa na kuteketea. Yerusalemu mpya ni imara na salama, kwa kuwa waumini wamejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii (Efe 2:20). Awezaye kuingia hapo ni yule tu anayeiamini Injili ya Bwana Yesu tuliyoipata kutoka kwa mitume wake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/