Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Siku ile Mungu atakapokaa pamoja na wanadamu kwenye mbingu mpya na dunia mpya ni uzuri ulioje! Kilio, machozi, huzuni na mauti vimekoma. Mungu mwenyewe atavikomesha. Atafuta kila chozi katika macho yao (m.4). Katika Yesu Kristo, aliye Alfa na Omega, watu wake hutoshelezwa katika mema yote na kufanywa wapya, akiwapa ya chemchemi ya maji ya uzima, bure (m.6). Je, habari hiyo haikuvutii sasa kushiriki? Ni yapi yakuzuiayo kupokea baraka na uzima? Zingatia yaliyoandikwa katika m.8, Waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na nao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Waonaje? Hayo yana maana gani, sasa na siku hiyo? Heri umwamini Bwana Yesu upate ushindi huo wa milele.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/