Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Mambo makuu mawili yameandikwa wazi: 1) Mungu atawahukumu wote sawasawa na matendo yao ambao hawakuandikwa katika kitabu cha uzima. Watatupwa katika lile ziwa la moto (m.14). Ni mfano wa adhabu ya milele ya Mungu. 2) Mungu atamwondoa adui wa mwisho, yaani, Mauti na Kuzimu. La tatu, ambalo halijaandikwa moja kwa moja, ni mwisho wa walioandikwa katika kitabu cha uzima. Ni nani hao? Wote waliomwamini Bwana Yesu. Watapewa uzima wa milele, kwa sababu wameandikwa katika kitabu kile kilicho kitabu cha uzima ni cha Mwana-Kondoo (Ufu 21:27).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/