Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Somo lasimulia mwisho wa vita kati ya Kristo Yesu na mpinga Kristo (= yule mnyama). Hatima ya huyo na nabii wa uongo ni kutupwa katika ziwa la moto ”wangali hai” (m.20; habari hii yaonyesha hukumu ya Mungu ni ya milele). Na jeshi lote la waliodanganywa na shetani kupitia kwa huyo mnyama na nabii wa uongo, litaangamizwa kwa neno la Bwana Yesu. Ni kazi bure kumpinga Yeye aliye mshindi daima. Kama ilivyoandikwa katika m.21, Wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake. Kumbuka, haya hayana budi kuwako upesi (Ufu 1:1). Salama yako na yangu ni kwa Yesu tu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/