Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Ni nani huyu aliyepanda farasi mweupe, na majeshi ya mbinguni wakamfuata, ambaye aitwa ”Mwaminifu” na ”Wa-kweli?” Ni Kristo Yesu. Tunapata uhakika huo katika m.13 ambapo imeandikwa kuwa jina lake aitwa, Neno la Mungu. Kumbuka jinsi Yesu anavyoitwa Neno katika Yn 1. Sifa na kazi za Yesu ni nyingi. Atakuja kuuhukumu ulimwengu kwa haki. Ni maana ya mfano unaosema kwamba atawachunga [mataifa] kwa fimbo ya chuma (m.15). Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani (Isa 9:6-7). Kwa kweli ni Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana awezaye kutekeleza hasira ya Mungu juu ya maadui wake wote. Basi, kama ukitaka kuwa mtu wa milki yake huyu ajaye kutawala, wakati mzuri kumwamini ni sasa! Maana tukingoja mpaka atakapotokea, tutajikuta tumechelewa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/