Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Katika somo la leo, Mbinguni kumejaa Haleluya tele na mashangilio mengi. Kwa nini? “Haleluya,” maana yake ni “Asifiwe Yehova.” Ni itikio la furaha ya moyoni kabisa la waliokombolewa kwa jinsi Mungu alivyoonyesha wokovu wake: Kwanza amekomesha kabisa Babeli, utawala wa mpinga Kristo. Pili furaha yao ipo hasa kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, nao watakuwa pamoja milele na Yesu, mpendwa wao, bila chochote kuwazuia. Haleluya! Je, umejiandaa kama mke wa Mwana-Kondoo alivyojiweka tayari? Basi, Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake (m.7).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/