Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Somo lahusu kuanguka kwa Babeli mkuu. Babeli mkuu ni nini? Ni mfano wa utawala wa mpinga Kristo unaojengwa katika habari za kihistoria za mnara wa Babeli (ukiwa na nafasi, ujisomee Mwa 11:1-9). Hutawaliwa na juhudi za kujitumainia na kumpinga Mungu (mist.3 na 7 yaonyesha sifa zake zilizo pamoja na “uasherati”, “kiburi”, “kwa kadiri yalivyojitukuza na kufanya anasa”). Watu wa Mungu wafanye nini ili wapone hukumu juu ya Babeli? Tokeni kwake (m.4)! Yaani tusishiriki dhambi zake, bali tupigane na matendo yake, na tukumbuke kuwa maumivu yake yatakuwa mengi kama vile utukufu wake ulivyo mwingi sasa. Atateketezwa kabisa kwa moto (m.8).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/