Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Kweli ya Mungu ikidhihirika yabadilisha yote yanavyoonekana. Kwa macho na akili ya kibinadamu twaweza kuona na kuelewa machache tu. Bila shaka sehemu ya kilichomshangaza Yohana ni kuona falme alizofikiri ni za kusaidia wanadamu zimebeba na kutegemeza taasisi inayowaua mashahidi watakatifu wa Bwana Yesu. Tena kwamba asili na chanzo cha hizo falme ni kuzimu. Tafuta daima kuyaona yote kwa mtazamo wa Neno la Mungu upate kweli yote: Mpinga Kristo yupo tu kuelekea kwenye uharibifu. Yule mnyama ... alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanga kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu (m.8).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/