Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - LukaMfano

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

SIKU 10 YA 20

Yesu anapojiandaa kuelekea Yerusalemu, anawatuma wafuasi wake kwenda kuandaa kila mji anaopanga kupitia. Wanaondoka bila chochote, hawabebi mizigo wala mikoba ya pesa, na wanakwenda wakiwa na nguvu za kuponya na ujumbe kuhusu Ufalme wa Mungu. Hii inaendelea kutuonyesha kuwa wafuasi wa Yesu ni watendakazi katika kazi ya Mungu ulimwenguni. Yesu anahubiri habari njema ya Ufalme, na wanaoiamini hawaipokei tu, wanajiunga naye katika kuieneza kwa wengine. Hii ndiyo njia ya Ufalme. Haihusiani na kupata mamlaka na utajiri wa ulimwengu huu; bali inahusu kupokea baraka za mbinguni ili kubariki ulimwengu. Hivyo, kwenye sehemu hii inayofuata, Luka anasimulia mafundisho ya Yesu kuhusu kumtegemea Mungu. Yesu anafundisha kuhusu kuomba, kutumia rasilimali ipasavyo na kuwa wakarimu. Mafundisho yake yanawapa furaha maskini na wanaoteseka. Lakini viongozi wa dini wanaghadhabishwa wanapomsikia Yesu akikosoa maisha yao ya tamaa, na wanaanza kupanga njama dhidi yake.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

•Kwenye mfano alioutumia Yesu, mtu aliyeibiwa alikuwa akisafiri kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko, hivyo huenda wasikilizaji wangechukulia kwamba alikuwa anatoka mji mkuu wa Israeli na hivyo ni Myahudi. Viongozi wa dini ya Kiyahudi, ambao ungetarajia wamsaidie, wanampita na kwenda zao. Mtu pekee aliyemsaidia Myahudi huyo alikuwa Msamaria. (10:25-31)

•Kwa kufahamu kuwa Wasamaria walidharauliwa na Wayahudi, unafikiria ni kwa nini Yesu alitaja hili kwenye simulizi yake? Je, hili linapanua vipi ufahamu wako kuhusu maana ya “mpende jirani yako?”

•Je, yuko mtu mwenye uhitaji anayekudharau? Je, umepokea lipi unaloweza kushiriki? Je, ni hatua ipi unayoweza kuchukua wiki hii ili kusaidia na kuonyesha upendo kwa jirani yako?

Ufalme wa Mungu unahusu kupokea baraka za mbinguni ili uweze kuzitoa kwa wengine bila kipimo. Hivyo wafuasi wa Yesu wanapaswa kujitenga na vishawishi na kuamini (10:42) kuwa Mungu ndiye anayetoa na ndiye anayejua jinsi ya kuwapa wana wake yaliyo mema (11:1-13). Yesu anafafanua kuwa karama njema ya Mungu ni Roho Mtakatifu (11:13) na ni karama ya kushiriki na wengine (11:5-6).

•Je, umewahi kumwomba Mungu kitu fulani lakini ukapokea kitu kingine badala yake? Je, Mungu alipokujibu ilileta vipi msaada, faraja na mafundisho ya Roho Mtakatifu maishani mwako? Je, baraka yake ilikuwezesha vipi kujitolea kwa wengine walio karibu nawe kupitia njia wasizotarajia?

•Kusoma na kutafakari kwako kukuchochee kuomba. Nena na Mungu kuhusu msukumo wako. Kiri kuhusu kuvunjika moyo kwako. Mwombe unachohitaji ili uweze kushiriki upendo wa Mungu wiki hii.

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Shirika la BibleProject liliandaa mwongozo wa Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio Sehemu ya 1 kuwahimiza watu binafsi, vikundi vidogo na familia kusoma kitabu chote cha Luka kwa siku 20. Mwongozo huu unajumuisha video za katuni, muhtasari wa uchambuzi na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia wahusika kumfahamu Yesu na kufuatilia mtiririko wa mawazo ya Luka pamoja na kuyaelewa mafunzo yake.

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com

Mipango inayo husiana