Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - LukaMfano

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

SIKU 13 YA 20

Kwenye sehemu hii inayofuata ya kitabu cha Luka, Yesu anasimulia simulizi inayoonyesha jinsi Ufalme wake unavyogeuza mambo ulimwenguni kwa njia ya kipekee, hii hapa simulizi yenyewe.

Kuna tajiri mmoja mwenye mavazi ya bei ghali na ana nyumba yenye uzio. Na kuna maskini mmoja mwenye vidonda, aitwaye Lazaro, anayeketi kwenye lango la yule tajiri, naye anatamani siku zote kula makombo yaliyoanguka kwenye meza ya yule tajiri. Lakini yule tajiri hampi chochote, na hatimaye wote wanakufa. Lazaro anapelekwa mahali pa faraja ya milele, naye yule tajiri anapelekwa mahali pa mateso. Kwa namna fulani tajiri yule anaweza kumwona Lazaro, na anapomwona tu, anaomba Lazaro atumwe ampe matone ya maji ili yamfariji. Lakini tajiri anaambiwa kuwa alichopendekeza hakiwezekani, kisha anakumbushwa kuhusu maisha yake ulimwenguni, jinsi alivyoishi maisha ya raha naye Lazaro alihitaji msaada wake kipindi hicho. Tajirihuyo anaomba Lazaro atumwe kwa ndugu zake ulimwenguni awaonye ili wasije wao pia wakafika mahali pa mateso. Lakini anaelezwa kuwa jamaa zake wameonywa vya kutosha kupitia maandiko ya manabii wa Kiebrania. Tajiri yule anasisitiza kuwa Lazaro akifufuka kutoka kwa wafu jamaa zake watashawishika. Lakini anaelezwa kuwa haiwezekani. Wanaokataa kumsikiliza Musa na manabii hawatashawishika hata mtu akifufuliwa kutoka kwa wafu.

Baada ya kusimulia simulizi hii, Yesu anawaonya watu wote kuhusu mateso yatakayowafikia wale wanaosababisha wengine kuteseka. Ili kuepuka mateso haya, anawafundisha watu wote kujaliana na kuwarekebisha wanaopotoka. Wanaosikiliza pale wanaporekebishwa watasamehewa, hata ikiwa wanahitaji msamaha huo tena na tena. Yesu ni mwenye rehema. Angependa watu wote wamsikilize kabla ya muda kuyoyoma. Yesu alikuja kuondoa mateso lakini kivipi? Anafundisha ukweli na anatoa msamaha wake kidhabihu kwa wote wanaoupokea. Vilevile, wafuasi wake wanapaswa kuwafundisha wengine na kuwasamehe.

Wanafunzi wa Yesu wanayasikia haya yote na wanagundua kuwa hawamwamini Mungu vya kutosha kiasi cha kuwawezesha kutekeleza mafundisho ya Yesu, hivyo wanaomba kuwa na imani zaidi.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

•Soma kwa undani hadithi iliyosimuliwa na Yesu katika Luka 16:19-31. Je, hadithi iliyosimuliwa na Yesu inahusiana na inakusaidia vipi kuthamini mafundisho yake katika Luka 17:1-4? Je, ungekuwa mhusika kwenye hadithi, unafikiri Yesu angefafanua vipi uhusiano wako na Lazaro na yule tajiri?

•Fikiria kuhusu mafundisho ya Yesu katika Luka 17:3. Unapaswa kufanya nini mtu anapokukosea? Je, kumkosoa mtu kwa upole ni kitendo cha upendo kivipi? Je, kwa nini ni vigumu sana kufanya hivyo? Fikiria kuhusu tukio ambapo mtu alikukosoa na akakusamehe. Ilikuwa vipi?

•Je, unahitaji msamaha wa nini? Je, ni nani anahitaji msamaha wako?

•Kusoma na kutafakari kwako kukuchochee kuomba. Mshukuru Mungu kwa maonyo yake ya upendo na ya wakati, omba msamaha kwa mambo uliyotenda ambayo huenda yaliwakwaza wengine, wasamehe waliokukosea na uombe imani unayohitaji ili uweze kujiunga kwenye mwito wa Yesu wa kuondoa mateso ulimwenguni.

siku 12siku 14

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Shirika la BibleProject liliandaa mwongozo wa Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio Sehemu ya 1 kuwahimiza watu binafsi, vikundi vidogo na familia kusoma kitabu chote cha Luka kwa siku 20. Mwongozo huu unajumuisha video za katuni, muhtasari wa uchambuzi na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia wahusika kumfahamu Yesu na kufuatilia mtiririko wa mawazo ya Luka pamoja na kuyaelewa mafunzo yake.

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com