Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - LukaMfano

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

SIKU 17 YA 20

Kabla hatujaanza somo la leo, hebu tuchambue sura ya tisa, ambapo Luka anafunua mpango wa kushangaza wa Yesu kutawala Israeli kwa kuwa mtumishi mwenye kuteseka anayerejelewa katika kitabu cha Isaya sura ya 53. Luka anatuambia jinsi Eliya na Musa walivyozungumza na Yesu kuhusu kuondoka kwake au “kutoka.” Yesu ndiye Musa wa kizazi hiki, ambaye kupitia kutoka kwake (kifo), atawakomboa Israeli kutoka kwenye utawala wa dhambi na uovu wote. Baada ya ufunuo huu wa kushangaza, Luka anaanza hadithi kuhusu safari ndefu ya Yesu kwenda mji mkuu kwa ajili ya Pasaka, ambako atakufa ili atawazwe kuwa Mfalme wa kweli wa Israeli.

Basi sasa, tukiangazia sura ya 22 leo, tunaona kuwa Yesu amewasili Yerusalemu kusherehekea sikukuu ya Pasaka ya kila mwaka──maadhimisho ya Kiyahudi ya kusherehekea jinsi Mungu alivyowakomboa wana wa Israeli kutoka utumwani. Yesu anapowakusanya wanafunzi wake kumi na wawili kwa chakula cha kawaida cha Pasaka, anafafanua maana ya mkate na kikombe kwa njia ambayo wanafunzi wake hawakuwa wamewahi kusikia, lakini maana yenyewe ndiyo inayoashiriwa kwenye simulizi ya Kutoka. Anawaeleza wanafunzi wake kuwa mkate uliovunjwa unaashiria mwili wake nayo divai inaashiria damu yake, ambayo itaanzisha agano jipya kati ya Mungu na Israeli. Katika hili, Yesu anatumia sakramenti ya Pasaka kueleza maana ya kifo chake kinachokuja, lakini wanafunzi wake hawaelewi. Mara ghafla wanaanza kubishana kwenye meza kuhusu ni nani atakayekuwa mkuu zaidi katika Ufalme wa Mungu, na baadaye usiku huo wanalala badala ya kuomba pamoja na Yesu. Mmoja wa wanafunzi hao kumi na wawili anakuwa mshiriki katika mauaji ya Yesu, na mwanafunzi mwingine anamkana Yesu.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

•Yesu anapindua kabisa hadhi ijayo kwa vyeo na anapindua maadili ya ulimwengu huu. Katika Ufalme wake, Mfalme hatafaulu vitani kwa kuua ili kuteka maeneo na kutwaa enzi, badala yake atauawa na kufa kama mtumishi mwenye kuteseka. Vivyo hivyo, viongozi katika Ufalme wake hawakandamizi wengine ili kufika kileleni, badala yake wanawatumikia wengine zaidi ya wanavyojitumikia (soma 22:24-27). Hili linakutia moyo au kukupatia changamoto vipi leo?

•Soma Luka 22:28-30. Ingawa Yesu anajua kuwa wanafunzi wake watajikwaa hivi karibuni, bado anafanya tangazo hili la kushangaza! Je, unajifunza nini hapa? Na Je, hili linakufunza nini kuhusu Yesu na Ufalme wake?

•Je, una uoga kama wa Petro (soma 22:33)? Je, kujitolea kwako kwa Yesu kumejaribiwa vipi? Je, umepotea njia vipi (soma 22:54-62)? Je, maombi ya Yesu kwako yametimia vipi? Umejifunza nini katika haya yote, na unawezaje kushiriki kile ulichojifunza na wengine ili kuwaimarisha (soma 22:32)?

•Kusoma na kutafakari kwako kukuchochee kuomba. Mshukuru Yesu kwa kupitia mateso ili kuwakomboa wanadamu kutoka katika utumwa wa dhambi, kiri udhaifu wako katika kupokea au kupata uhuru huu na unachohitaji leo.

Andiko

siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Shirika la BibleProject liliandaa mwongozo wa Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio Sehemu ya 1 kuwahimiza watu binafsi, vikundi vidogo na familia kusoma kitabu chote cha Luka kwa siku 20. Mwongozo huu unajumuisha video za katuni, muhtasari wa uchambuzi na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia wahusika kumfahamu Yesu na kufuatilia mtiririko wa mawazo ya Luka pamoja na kuyaelewa mafunzo yake.

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com

Mipango inayo husiana