Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - LukaMfano

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

SIKU 19 YA 20

Luka anatueleza kuhusu baadhi ya wanawake waliokuwa wafuasi wa Yesu alipokuwa hai. Wanauona mwili wa Yesu ukiwekwa kaburini siku ya kuuawa kwake, na wanarudi asubuhi ya siku inayofuata Sabato, mapema iwezekanavyo. Lakini wanapofika, wanakuta kaburi likiwa wazi na tupu. Hawafahamu mwili wa Yesu umekwenda wapi, na ghafla malaika wawili waliovaa nguo za kumeta-meta wanawatokea na kuwaambia kuwa Yesu yu hai. Wanashangaa. Wanakimbia na kuwaambia wanafunzi wengine kila kitu ambacho wameona, lakini ripoti yao inachukuliwa kuwa upumbavu na hamna anayewaamini.

Wakati huo huo, nje ya Yerusalemu watu wawili miongoni mwa wafuasi wa Yesu walikuwa wanaondoka mjini kuelekea mji wa Emau. Wanazungumza kuhusu yaliyotukia wiki ya Pasaka. Yesu anawakaribia na kuanza kuongozana nao lakini hawamfahamu. Yesu anazungumza nao na kuwauliza wanachozungumzia. Wanasimama, wanafedheheshwa na mazungumzo hayo na pia wanashangazwa kwamba hakuwa anafahamu yaliyotokea siku chache zilizopita. Wanamwambia wanamzungumzia Yesu, nabii mwenye uwezo waliyedhaniangeiokoa Israeli lakini akauawa. Wanamwambia jinsi wanawake fulani wanashuhudia kuwa yuko hai, lakini hawajui cha kuamini. Yesu anawaeleza kuwa hilo lililotokea ndio limekuwa likiashiriwa kwenye Maandiko ya Kiyahudi. Israeli ilihitaji Mfalme ambaye angeteseka na kufa kama mwasi kwa niaba ya waasi wote. Mfalme huyu angethibitika kupitia ufufuo wake ili kutoa uzima wa kweli kwa wale wanaoupokea. Lakini wasafiri hawa bado hawaelewi. Wamekanganyika sana na wanamsihi Yesu akae nao kwa muda zaidi. Hili linatupeleka paleLuka anapotueleza jinsi Yesu alivyoshiriki nao chakula. Anautwaa mkate, anaubariki, anaumega na kuwapa kama alivyofanya kwenye karamu ya mwisho kabla ya kifo chake. Hii inaashiria jinsi mwili wake ulivyovunjwa, yaani kifo chake msalabani. Na wanapokula mkate uliomegwa macho yao yanafunguliwa ili wamwone Yesu. Hiki ni kisa kinachohusu ugumuwakumtambua Yesu ni nani. Je, iweje nguvu za kifalme na upendo wa Mungu zidhihirishwe kupitia kifo cha aibu cha mtu huyu? Je, mtu mnyenyekevu anawezaje kuwa Mfalme wa ulimwengu kupitia udhaifu na kujitoa kama dhabihu? Ni vigumu sana kuelewa! Lakini huu ndio ujumbe wa Injili ya Luka. Mawazo yetu yanahitaji kufanywa upya ili tuweze kuelewa na kuupokea Ufalme wa kipekee wa Yesu.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

•Pata picha upo kwenye kaburi la Yesu siku ya kufufuka kwake. Je, ungehisi vipi? Ungesema na kufanya nini?

•Je, unaona jinsi manabii wote wa kale wanavyomwashiria Yesu? Je, unaamini kuwa Yesu ni Mfalme? Ikiwa unaamini, kumbuka wakati ambapo hukuwa unamwamini. Je, ni nini kilichokusaidia kumtambua Yesu ni nani? Na ikiwa bado huiamini simulizi ya Luka kuhusu maisha ya Yesu, mwombe Mungu leo akuwezeshe kuona na kuelewa Yesu ni nani.

•Kusoma na kutafakari kwako kukuchochee kuomba kutoka moyoni. Anakusikia.

siku 18siku 20

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Shirika la BibleProject liliandaa mwongozo wa Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio Sehemu ya 1 kuwahimiza watu binafsi, vikundi vidogo na familia kusoma kitabu chote cha Luka kwa siku 20. Mwongozo huu unajumuisha video za katuni, muhtasari wa uchambuzi na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia wahusika kumfahamu Yesu na kufuatilia mtiririko wa mawazo ya Luka pamoja na kuyaelewa mafunzo yake.

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com

Mipango inayo husiana