Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - LukaMfano

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

SIKU 16 YA 20

Yesu anaposubiri sherehe ya Pasaka akiwa Yerusalemu, anafundisha kila siku hekaluni kuhusu asili ya Ufalme wa Mungu na mambo yatakayofanyika baadaye. Wakati mmoja, Yesu anatazama na kuwaona matajiri wengi wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina ya hekalu na mjane mmoja maskini anatia mle ndani senti mbili pekee. Yesu anajua kuwa matajiri hao walitoa kutokana na wingi wa mali yao, bali mjane alitoa vyote alivyokuwa navyo. Kwa hivyo anazungumza na kuwaeleza wote wanaomsikiza, “huyu mjane maskini ametoa zaidi kuliko wote.”

Yesu sio kama wafalme wengine wanaothamini matajiri kwa sababu ya michango yao mikubwa. Katika Ufalme wake, watu hawahitaji kuwa na mali nyingi ili waweze kutoa zaidi. Yesu anafundisha kuwa utajiri wa ulimwengu huu una mwisho na mwisho wake umekaribia lakini pia anasema kwamba Ufalme wake umekaribia, kwa hivyo anawaambia wafuasi wake waweke mioyo yao mbali na hali ya wasiwasi na mali ya ulimwengu na badala yake wamtegemee yeye (kifungu cha 21:13-19, 34-36).

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

•Fikiria jinsi Yesu anavyoweza kuthamini sarafu mbili za shaba zaidi ya mchango mkubwa wenye thamini ya juu. Je, hii inakueleza nini kuhusu asili ya Ufalme wake?

•Tafakari kuhusu onyo la busara la Yesu katika Luka 21:34-36. Je, kifungu hiki kinakufunza nini kwa sasa? Utatekeleza vipi mafundisho ya Yesu wiki hii?

•Yesu anamnukuu nabii Danieli katika Luka 21:27. Soma Danieli 7:13-14. Unagundua nini?

•Kusoma na kutafakari kwako kukuchochee kuomba. Nena na Mungu kuhusu ukuu wake, kiri kuhusu muda au pesa ulizotumia hovyo kwenye tamaa za vitu vya dunia na umwombe unachohitaji ili uelekeze upendo wako kwa Ufalme wa Yesu.

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Shirika la BibleProject liliandaa mwongozo wa Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio Sehemu ya 1 kuwahimiza watu binafsi, vikundi vidogo na familia kusoma kitabu chote cha Luka kwa siku 20. Mwongozo huu unajumuisha video za katuni, muhtasari wa uchambuzi na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia wahusika kumfahamu Yesu na kufuatilia mtiririko wa mawazo ya Luka pamoja na kuyaelewa mafunzo yake.

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com

Mipango inayo husiana