Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano
Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? (m.34) Ujumbe wa malaika ulipita akili ya Mariamu. Alishindwa kuelewa, maana kuchukua mimba bila mwanamume haiwezekani kabisa. Jibu la Gabrieli ni kwamba hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu (m.37). Huwa Mungu anapotenda matendo makuu ya kuwaokoa wanadamu, pia hufanya miujiza mikubwa. Ila huu unapita miujiza yote. Maana ni Mungu mwenyewe aliyeshuka kwetu wanadamu. Mwana wake alifanyika mwili (Yn 1:14, Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu). Ni binadamu na Mungu katika mtu mmoja: Yesu! Maneno ya malaika yanaeleza vizuri, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu (m.35).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/