Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022

SIKU 6 YA 30

Somo la leo linatupa picha ya mbinguni ilivyo na itakavyokuwa: Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote. Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao (m.1-3). Yote yanayotendeka sasa hapa duniani yanalenga kwamba watu kutoka pande zote za dunia watasimama mbele za Mungu, wakiwa watakatifu. Ndivyo walivyo kwa sababu walikombolewa kwa damu ya Mwana-Kondoo, yaani Kristo Yesu. Mbinguni wana kazi moja tu, nayo ni kumwabudu na kumhimidi Mungu. Jiulize: Je, wewe utakuwa miongoni mwao? Mpe Yesu maisha yako.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/