Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano
Walikawia sana kurudi Misri, maana Israeli hakutaka kabisa Benyamini aende huko. Kwa masikitiko akasema, Mwanangu hatashuka pamoja nanyi, maana nduguye amekufa, naye amesalia peke yake; mabaya yakimpata katika njia mtakayoiendea ndipo mtakaposhusha mvi zangu kwa sikitiko mpaka kaburini (42:38). Simeoni huenda alianza kuhangaika huko gerezani! Ila walipokwisha kula nafaka, Israeli alilazimishwa kuwatuma tena, akisema, Rudini huko, mkatununulie chakula kidogo (m.2). Yuda alionekana kuwa ni kiongozi kati ya ndugu zake. Yeye ndiye aliyezungumza na baba yake kwa niaba ya wote. Alimwambia, Yule mtu alituagizia sana akisema, Hamtaniona uso wangu, ndugu yenu asipokuwa pamoja nanyi … Kwa hiyo, mpeleke kijana pamoja nami, tuondoke, tuende zetu, ili tupate kuishi, wala tusife, sisi na wewe na watoto wetu (m.3 na 8; ling. 37:26-27 kuhusu Yuda alivyoongoza mauzo ya Yusufu akisema, Kwafaa nini kumwua ndugu yetu, na kuificha damu yake? Haya, na tumwuze kwa hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu ... ). Sasa huonyesha roho tofauti: Mpeleke kijana pamoja nami ... Mimi nitakuwa mdhamini wake, umtake mkononi mwangu (m.8-9).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/