Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano
Walipomimina magunia yao, kumbe! bahasha ya fedha ya kila mtu imo katika gunia lake (m.35). Tukio hili ni dalili kwamba Yusufu bado aliwapenda. Dalili nyingine ni kulia kwake wakati aliposikia jinsi ndugu zake walivyojuta kwa tendo lao la kumwuza yeye. Ndipoakajitenga nao akalia. Kisha akawarudia, na kusema nao (m.23-24). Yusufu alikuwa na uwezo wa kuwalipa kisasi ndugu zake, lakini hakutaka kufanya hivyo. Alikuwa amewasamehe. Ndiyo maana akasema, Msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu. Mungu alinipeleka mbele yenu kuwahifadhia masazo katika nchi, na kuwaokoa ninyi kwa wokovu mkuu. Basi si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri
(45:4-10)! Ukali wake ni kutokana na hamu yake ya kumwona mdogo wake! – Je, hatutaki kuwasamehe waliotukosea?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/