Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano
Mkamlete ndugu yenu mdogo kwangu; hivyo maneno yenu yatahakikishwa, wala hamtakufa (m.20). Yusufu alitaka kuwajaribu ndugu zake ili ieleweke wazi kama bado ni wadanganyifu au ni wasema ukweli. Mtabainika kwa njia hii (m.15), yaani, watajulikana wazi walivyo. Na kuna dalili kwamba wamebadilika, maana baada ya kuamriwa hivyo wakaambiana: Kweli sisi tulimkosa ndugu yetu ... kwa hiyo shida hii imetupata (m.21). Mioyo yao si migumu tena bali imelainika. Walijisikia kushitakiwa. Zingatia ilivyoandikwa katika Ebr 3:15: Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/