Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano
Leo twasoma mwanzo wa habari jinsi Yusufu alivyokutana tena na ndugu zake, na kisha alivyopatana nao (Mwa 42-45). Ni masimulizi yanayovutia sana! Yusufu akawatambua nduguze, bali wao hawakumtambua yeye (m.8). Tukumbuke kwamba walipomwuza alikuwa kijana mdogo tu wa miaka 17 hivi (37:2, Yusufu, aliyekuwa mwenye miaka kumi na saba, alikuwa akichunga kondoo pamoja na ndugu zake). Lakini sasa ni mwenye miaka 30 aliposimama mbele ya Farao (41:46). Tena, Yusufu alivaa nguo mpya na kukata nywele zake kabla hajaruhusiwa kuonana na mfalme wa Misri (41:14). Bila shaka aliendelea na mtindo huu wa kimisri alipoanza kutawala nchini. Kwa hiyo tusishangae kwamba ndugu zake hawakumtambua. Pia alijifanya kama mgeni kwao kwa kuamua kuongea nao kwa kumweka mkalimani kati yao (42:7, 23).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/